Wednesday, 5 January 2011

HAPPY BIRTHDATE SWEET DADY.




Kwanza namshukuru Maanani kwa kuweza kutuvusha mwaka uliopita na kutufikisha mwaka huu wa 2011. Ni mengi sana tumepitia ambayo si kwa uweza wetu bali ni kwa nguvu zake tumewaza uona mwaka huu.

Pia nipende kumshukuru Mungu kwa kunipa wazazi hawa na hapa nianDikapo napenda  kukupongeza sana Baba kwa kukumbuka siku yako ya kuzaliwa.

Sisi kama wanao twajivunia sana kuwa nawe na Mama, umetufunza mengi ambayo sasa twaonekana kuwa kioo katika jamii na hata yanayotufanya kuishi vizuri na wenzetu ilhali tukiendeleza ule "UPENDOmlioturithisha. Twajivunia kuwa na Wazazi kama nyinyi na twawaombea Baraka zaidi na maisha marefu ili muwezeona nini matunda ya malezi meme kwa wanenu katika yale mliowafundisha. WE WILL ALWAYS BE PROUD OF YOU  na kwa pamoja twakutakia heri na fanaka katika kuikumbuka siku yako hii ya kuzaliwa.


“It is a wise father who knows his own child.” 
                      William Shakespeare.

SWEET DADY.

HAPPY BIRTHDATE BABA.

4 comments:

  1. Umenifanya NISTAAFU kuandika sasa.
    Baba ataendelea kuwa akilini kuliko manenoni.
    Can't say enough. Labda niseme tu kuwa NAJIVUNIA KUWA MWANAE NA HATA SIKU MOJA SIJAWAHI JUTIA KUKULIA KWAKE.
    Najivunia alivyotuunganisha na wanandugu na anavyotufanya tuwe tulivyo.
    Well!! Ni baba ambaye anaishi na Mama ambaye naye ni wa muhimu saaaaana. Kama si wao KUVUMILIANA, KUPENDANA NA KUHESHIMIANA na pia kuendelea kuwa wapendwa kwa namna walivyo, labda mambo yangekuwa tofauti, lakini UKWELI NI KWAMBA KWA PAMOJA WANATENGENEZA FAMILIA BORA KULIKO UBORA WENYEWE.
    TATIZO MOJA nililoona kwa Baba huyu (pamoja na Mama), walinifanya niaminikuwa ndoa ni kitu rahisi, kisicho na mabonde wala malumbano. Ni kwa kuwa sikuwahi kusikia wakibishana ama kuonesha kutoelewana, nami nikahisi "maisha ni kama niyaonavyo kwa Baba na Mama".
    KUMBE SIVYO
    Sasa kama Mume, kama Baba na mlezi, naona mengi, naona yote na NAZIDI KUTOA SIFA NA SHUKRANI KWAO

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa baba.

    ReplyDelete