Sunday 30 October 2016

UJIO MPYA

Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniweka hai na kunipa nguvu. Ni kitambo sasa tokea nimetoka kijiweni na leo nimeona ni vema nirudi nikiwa na meengi ya kujadili na kushirikiana nanyi katika kuikuza na kuindeleza jamii yetu.
Awali nimekuwa najadili mambo kadha wa kadha yahusuyo Siasa na jamii lakini kwa sasa nitakuwa nagusia zaidi katika mambo yahusuyo "Jamii na afya ya Jamii". Lakini kabla ya kuanza nipende kwanza Kuwashukuru Familia, Ndugu Jamaa na Marafiki kwa uwezo wenu na michango yenu iliyoniwezesha kuwa hivi nilivyo leo hii. Kipekee nimshukuru Mke wangu mpendwa Nancy N. Bandio kwa kuwa na imani  namikatika meengi sana niliyopitia kufika hapa. Umekuwa kielelzo kikubwa cha mafanikio yangu na nipende kukushukuru kwa kunipenda.

Nakupenda sana Mama

Kwa kukeleza wewe hapatoshi lakini nizidi kuomba ushirikiano wenu wadau pia kila mwana afya ili tuweze kuelimishana meengi yahusuyo afya zetu ili kuwa na tanzania njema yenye kizazi chenye afya na maadili mema.


Tuko pamoja

Friday 17 February 2012

KERO YANGU NA BUKOBA YANGU


Kumekuwa na baadhi ya kero ambazo sijui kama zanikera mimi peke yangu ama ni wadau wengi pia zawakera, na moja ya mambo ambayo ni kero kwangu katika mji wangu wauitao manispaa ni MFUMO MBOVU wa ukusanyaji kodi za Halmashauri hasa za USAFI na PARKING  katika mji wa Bukoba.
Mkuu wa mkoa wa Kagera.

Tokea kuletwa kwa Mkuu wa mkoa mpya Kanali Mstaafu Ndugu Fabian Massawe, kumekuwa nahali ya dhati ya kuonekana kupatikana kwa mabadiliko katika Manispaa ya Bukoba hali ambayo nimekuwa nikiipenda japo naona kama imechelewa ila kwa wakati mwingine naamini kuwa imekuja katika muda muafaka kwani hata ujio wa taasisi za Elimu ya juu ndipo zaanza na nategemea kwa miaka kadhaa basi itakuwa na mafanikio na mabadiliko ya kweli kuonekana katika mkoa wenye sifa nyingi nje ila usio na yale wengi wanadhania kuwa nayo kwa sababu tu ya hali watu wa mkoa huu huonyesha wakiwa nje ya kwao.
Mh. Massawe tangu akiwa mkuu wa wilaya ya Karagwe amekua na  utaratibu maalum wa usafi katika wilaya hiyo katika siku ya Alhamis ambayo ilijulikana kama MASSAWE DAY ambayo hata alipopata ukuu wa mkoa amejitahidi kuisisitiza na kuifanya siku ya usafi hasa katika manispaa ya Bukoba.
Mh. Mkuu wa Mkoa. Ndg F. Massawe katika usafi

Tokea hapo, uongozi wa manispaa ukabuni mradi binafsi ambao kwa hakika ni kwa ajili ya kuwanufaisha wao wa kutoza pesa kwa ajili ya uegeshaji magari katika manispaa hali ambayo nadhani yanikera kuliko kitu chochote naweza sema.
 Kiutaratibu twajua kuwa kabla ya kuanzisha kitu ni vema kuandaa mazingira ili hata ukiiweka hicho kitu kiwe na manufaa kwako na kwa Umma, lakini wenzangu na mie hawa wamebuni kamradi binafsi haka na kutapakaza watu manispaa nzima wakitoza ushuru wa shilingi 500 kwa siku nzima bila hata kutoa elimu kwa "VIBARUA" hawa.
Parking za Manispaa zitozwazo kodi

Kwa kawaida tulitaraji kwanza kuona parking katika maeneo mbalimbali ndipo utoe elimu kwa Umma kuhusu pesa za parking na kuelimisha watoza ushuru wa Parking kujua ni baada ya muda gani wanastahili kumtoza mtu pesa. La kushangaza ni kwamba hakuna mahali popote katika manispaa ambapo pametengenezwa maalum kwa ajili ya parking ila Vibarua hawa wanatoza kodi na pangine hata kwenye maduka ambayo weenye majengo wanalipia kodi eneo lote.
Nikirudi kwenye suala la USAFI, huku nako naanza kuona dalili za kushindikana kwa jambo hili kwa kuwa watu hasa viongozi wa mitaa wamefanya hii programu kuwa kama njia ya kujipatia pesa za kiyabadili maisha yao. Nasema haya kwa sababu kuu moja nayo ni hii
Katikasiku za hivi karibuni, Serikali ilianzisha mfumo mpya wa kuweza kujikusanyia mapato kwa kutumia vifaa maalumu ambavo wafanya biashara na Taasisi nyingi wanavitumia lakini kwa Halmashauri ya Manispaa hawana. Tozo la parking wapewa kijilisiti ambacho hata mimi naweza forge na kusema ni mtoza kodi na hivyo pesa nyingi kuishia kwa hawa watoza kodi,
ELCT Central office Parking

Tuachane na hilo, katika suala zima la usafi kuna adhabu zinatolewa kwa wanaokiuka utekerezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa ambazo zinatofautiana kulingana na ukubwa wa kosa na taasisi ama familia ama Biashar lakini zikianzia 20000 kupanda ama kifungo cha miezi sita.
Pesa hizi zafika zitakiwako zikiwa zoote? Hilo ndilo swali hasa na Je? kama zafika zinatumika katika kazi gani? Maana ninauhakika kuwa hivi ni vyanzo mbadala vya mapato katika manispaa lakini twaenda leo na kuuliza matumizi ya vyanzo hivi vya mapato yakoje nina uhakika hakuna mwenye jibu

Friday 2 December 2011

UKWELI UKO WAPI?

Labda kwa vile nimo ndani ya moja ya nchi masikini kiuchumi hivyo naweza shindwa onyesha wazi ulipo ukweli juu ya maendeleo ya nchi hizi masikini Duniani.
Tokea kuwako kwa Kambi mbili zenye nguvu na zinazokinzana Duniani kambi ya mfumo wa nchi za kibepari na Kambi ya mfumo wa nchi za Kijamaa, kumekuwako na maonevu na unyonyaji mwingi sana dhidi ya nchi zinazoendelea ufanywao na mataifa makubwa na yenye nguvu kiuchumi.



Mgawanyiko wa kambi hizi mbili ulikuwako tokea mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 lakini ukaja kukua baada ya Vita vikuu vya pili vya Dunia ambapo kambi hizi mbili zilizidi pingana kiitikadi na kijeshi.

Kambi ya Kibepari iliongozwa na Marekani na kambi wa Kijamaa iliongozwa na Urusi. Katika kambi hizi, mataifa masikini yaliingizwa kwenye mikataba ya kujiunga na kambi moja wapo japo baadhi ya mataifa yalikataa kujiunga na kambi hizo na kuanzisha ushirikiano wan chi zisizofungamana na upande wowote.



Mataifa masikini, yamekuwa yakijaribu kutafuta uhuru wake wa kisiasa na kiuchumi kwa njia ya amani na utulivu, lakini yamekuwa yakiwekewa vikwazo vingi kutoka katika mataifa yale yaliyoendelea kiuchumi na kisiasa hata kufanyiwa maamuzi ambayo pengine yamediriki hata kwenda kinyume na Haki za Binadamu.



Nchi hizi (masikini) zimekuwa zikikosa msimamo wao thabiti na hata kubanwa kwa kila njia katika Nyanja za uchumi na siasa kwa kufanyiwa maamuzi. Kwa mfano kila tunachozalisha tunanauza kwa bei ya kupangiwa na ambayo ni ya chini sana katika soko la kimataifa na kila tunachonunua kikiwa ni cha bei Ghali. Kwa maana hiyo basi naweza sema kuwa Jitihada zote za nchi masikini za kutaka kujikomboa na kujitafutia maendeleo zinaonekana kuwa ni kazi bure kama hatutaweza kujitegemea na kuzidi kuzihusudu na kuzitegemea nchi tajiri zitusaidie katika kilio chetu cha kujiokomboa bila sisi wenyewe kuwa na mipango madhubuti na kuifanyia kazi.



Nchi changa hazina budi kuanzisha mikakati mbalimbali itakayowezesha kujikomboa kikamilifu. Kwa mfano uanzishwaji wa umoja wa soko nafuu wa bidhaa zetu, uimarishwaji wa njia za mawasiliano na uchukuzi, ulinzi wa pamoja hayo ni baadhi tu ya mbinu zinazoweza kusaidia katika kuleta ukombozi katika mataifa masikini.



Viongozi nao hawana budi kuungana kwa kauli na vitendo. Hakuna sababu ya kuyaogopa mataifa makubwa kiuchumi kwani kitendo hicho ndicho kinayafanya mataifa mengi Masikini kuwa vibaraka wa mataifa hayo.



Hivyo basi, Mataifa masikini kokote Duniani hatuna budi kuungana kwa hali na mali hadi tone la mwisholimekombolewa kutoka kwenye uonevu, mateso na kunyanyaswa na mataifa haya makubwa kiuchumi kwani

“MBINU ZA KUJIKOMBOA ZINAPATIKANA KWENYE UWANJA WA UKOMBOZI (MAPAMBANO)”.

Mapambano yakiendelea ushindi ni lazima.

Thursday 13 October 2011

HIVI NDIVYO SIKU YA PAULINA ILIKUWA

Mambo yakaanza hivi.
Tukiwa twamalizia siku hii ya leo siku iliyokuwa "maalyumu" kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtoto Paulina Arriana Bandio nipende kutoa shukrani kwa woote mlioshiriki nasi kwa namna moja ama nyingine kuiwezesha siku hii kufana kwa kiasi ilichofana.
Hongera Saana Mjukuu wetu. We are so Proud of You.
Hakika imefana hasa kwa sababu ameweza sherehekea sherehe hii akiwa na Mama, Babu, Bibi na Baba wadogo zake (Kakulu na Kato) Na pia kuweza jumuika na baadhi ya watoto wenzake katika sherehe hii.
Twaamini hii itakuwa kumbukumbu nzuri sana sio leo tu bali maishani mwake mwoote. Nasi twazidi muombea Baraka nyingi, Hekima, Upendo na Moyo wa huruma bila ya kusahau kumcha Mwenyezi Mungu aliye Muweza wa yoote.
Matukio mengine kwa ufupi ni kama yaonekanavyo hapo chini;
Wa kwanza nilishazima sasa ni zamu ya huu tena,
Hayaaaaaaa. Nazimaaaaa.
Wooow! I thank God I have made it, 
This is a special Cake for you BABU.
Asanteeeeee na Hongera sana mjukuu wa Jina.
This is for You Mummy. I love you so much.

Na hawa ndio Maswahiba wangu huku.
Asanteni nyote kwa kuwa nasi kwa namna moja ama nyingine katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto Paulina.
BARIKIWA.

HAPPY BIRTHDAY SUPER PAULINA.


The Little Angle (Napenda sana kumuita MAMA)
Ni jambo la pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukulinda hadi leo hii uadhimishapo miaka miwili tangu kuzaliwa kwako. Hakika ni safari ndefu ila twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake na hata kuweza fikia hapa.

Pia nitumie fursa hii kipekee kuwakaribisha sana Nyumbani Bukoba Tanzania Wewe (PAU) na Mama Pia.
Mama na Mwana. Karibuni Sana Bukoba wapendwa.
Twafurahi sana kujumuika nanyi katika sherehe hii na kuwa nanyi katika kipindi chote tutachobahatika kuwa nanyi.
 Hakika ni furaha sana kwetu sisi kama Familia na hata kwa kila mmoja wetu kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda safarini mpaka kuwafikisha salama na pia kuwashukuru ninyi kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali hadi kufikia Azma yenu ya kufika huku. Ujio wenu ni ishara tosha ya upendo wenu kwetu na si twaahidi kushirikiana nanyi katika kipindi chote tutachokuwa nanyi.
The Super Parents with their Angel P.A.B
Hivyo basi twawapenda na kuwaombea muwe na Afya tele na amani kwa kipindi chote tutakachokuwa nanyi huku tukimwombea pia kaka yetu Mubelwa (Baba Pau) azidishiwe afya njema na Baraka kwa kipindi choote tutakachokuwa nanyi na hata baada ya Hapo.

KARIBUNI SANA TANZANIA,

KARIBUNI SANA BUKOBA  MAMA PAULINA  NA PAULINA. 

Na mwisho niseme
HAPPY BIRTHDAY Pauliana Arianna Bandio. 

BARAKA KWENU NYOOTE.