Thursday, 10 February 2011

HIZI NI POLI-TRICKS.



Kaka yangu Mkubwa Mubelwa katika Blog yake anasegment  yake iitwayo "TANZANIA YANGU". Kiukweli naipenda sana na hujifunza na kucheka sana nionapo mambo ya kipuuzi yanayofanywa na Nchi yetu hasa kule BUNGENI. Siamini kama mambo serious yanaweza kujadiliwa kimasihara hivi ikiwa wabunge wamechaguliwa kuwawakilisha wanchi wa majimboni kwao.
Nilipokua nawaza kuandika kuhusu hilinakapata wazo kuwa ningesema TANZANIA YANGU INAYOMKANDA MBWA KIZAZI. Kwa nini nasema hivi? Wote twakumbuka dhahiri kuwa wakati Bunge likizinduliwa rasmi baada ya uchaguzi mkuu uliompatia ushindi Ndugu Jakaya M. Kikwete kuendelea kuongoza nchi kwa awamu ya pili na ya mwisho, Wabunge wa kambi kuu ya upinzani Bungeni (CHADEMA) walisusia kikao hicho na kuamua kutoka nje ya Bunge. Mengi yalisemwa na kuanza kusahaulika kama ilivyo kawaida ya Watanzania kusahau mapema ila kilichonisukuma hadi kuweka mawazo yangu kijiweni ni hali ya kushangaza ya Wabunge hao kukaa na kukubaliana na Hotuba ya Mh. Rais ilhali waliamua kutoka na kutoisikiliza. Kiukweli haikuniingia akilini na ndipo nikaanza amini kuwa Siasa sio mcheza mchafu ila wachezaji ndio wachafu. Kwa nini wawe wanafiki kiasi hicho sasa kama walijua watakuja kula matapishi yao? Na sasa nimegundua mbinu yao ya kugomea vikao na kutoka nje kisa wametofautiana kwa hoja na upinzani wenzao ama Chama tawala. Swali kwa hawa ndugu ni kwamba wanadhani kususa vikao na kutoka nje ni suluhisho la matatizo yao? Na wanawaza nini wakirudi majimboni na kuulizwa jinsi fani wamewawakilisha wananchi wao watajibu vp? Kwamba ni kwa kutoka kwenye vikao? Ila haya yote nayaona kama matokeo ya kuburuzwa kwa wanachama (wabunge) na Viongozi wa chama waliopo mjengoni na kuhamasisha migomo katika kutaka vuruga Amani wakijua wana watu wa kuwa support kutoka vyuoni. Na kama ndio njia za kushinikiza mabadiliko ya katiba kuwa ya haraka kama wanavyotaka naweza sema wataishia angukia pua kama tulivyoona vyama vya upinzani vilivyowahi kuleta upinzani kabla yao.

No comments:

Post a Comment