Picha kwa hisani ya Kaka FRANCIS GODWI |
Ikiwa ni muda mchache umepita tokea matokeo ya shule za sekondari kutangazwa, twaweza pata picha halisi ya elimu bora iliyoahidi Serikali Tukufu. Siwezi sema moja kwa moja kuwa hii ndio kudhihirisha usemi wa "MWANZO MGUMU" maana huu nauona kuwa mwanzo wa mwisho. Serikali baada ya kujenga majengo wakishirikisha baadhi ya wananchi alifanikiwa kayajenga katika kila kata kama mpango maalumu wa kuendeleza elimu Tanzania na kupata sifa kedekede kutoka kwa wafadhili wake kama UNESCO. Kwa kiwango kikubwa japo bila ya kusikiliza ni nini wananchi wake wanataka, Serikali imekua ikijichukulia maamuzi na kuendelea kuwakumbatia hao iwaitao wafadhili na kusahau kuwa "MTEGEMEA CHA NDUGUYE, HUFA MASIKINI."Kiukweli tunashindwa fanya maendeleo yetu kwa kuwa twadhani hao tunaowakumbatia NDIO WENYE MAJIBU SAHIHI YA MATATIZO YETU na kuwa wanania njema nasi lakini mimi nazidi amini bila sisi kujikana hatufiki kokote. Tuachane na Hayo, Takribani miaka minne iliyopita, Shule nyingi za kata al maarufu kama YEBOYEBO zilifunguliwa kwa nia Nzuri tu ya kutoa elimu kwa Watanzania ila sasa matokeo yametoka ni AIBU. hii ni kwa kuwa serikali ilijiandaa kutengeneza majengo wakidhani ndio maana halisi ya Shule, mengi ya majengo hayo hayakuwa na vifaa vya kufundishia wala waalimu hali iliyowalazimu hata wale walioteuliwa kwenda kwenye hizo shule kugoma. Sijui ila nipende tu pia naweza sema hili ya kuwa udhaifu ulioonekana ndio nahisi ulitumiwa na serikali kufuta Mitahani ya Kidato cha pili ilhali hawa waliomaliza wakiwa kidato cha pili (Form two) ili kutoyaibua hayamapema ile na serikali kuoekana kushindwa kusudio lake hivyo kuamua kuwapitisha kiholela ili yanapokuja tokea yaliyotokea wao watakuwa madarakani tena na kwa hilo wamefanikiwa. Ila hofu yangu kubwa ni kwamba tuliwapitisha kiholela na kidogo wamejua "How are you," Je? s\Si hawa ndio wataongoza mapinduzi ya kisiasa miaka ijayo ama ndo kama CULTURE ya Mtanzania kusahau? Sitaki waza kwa niaba ya wengine kuhusu hili ila tu nilikua nataka toa angalizo kuwa "MPANGO WA SASA NI KUJENGA ZAHANATI ZA KATA, JE? NA ZENYEWE SI ZITAUA KAMA SHULE ZA KATA ZILIVYOFELISHA?
TUONANE MUNGU AKIPENDA.
No comments:
Post a Comment