Friday, 2 December 2011

UKWELI UKO WAPI?

Labda kwa vile nimo ndani ya moja ya nchi masikini kiuchumi hivyo naweza shindwa onyesha wazi ulipo ukweli juu ya maendeleo ya nchi hizi masikini Duniani.
Tokea kuwako kwa Kambi mbili zenye nguvu na zinazokinzana Duniani kambi ya mfumo wa nchi za kibepari na Kambi ya mfumo wa nchi za Kijamaa, kumekuwako na maonevu na unyonyaji mwingi sana dhidi ya nchi zinazoendelea ufanywao na mataifa makubwa na yenye nguvu kiuchumi.



Mgawanyiko wa kambi hizi mbili ulikuwako tokea mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 lakini ukaja kukua baada ya Vita vikuu vya pili vya Dunia ambapo kambi hizi mbili zilizidi pingana kiitikadi na kijeshi.

Kambi ya Kibepari iliongozwa na Marekani na kambi wa Kijamaa iliongozwa na Urusi. Katika kambi hizi, mataifa masikini yaliingizwa kwenye mikataba ya kujiunga na kambi moja wapo japo baadhi ya mataifa yalikataa kujiunga na kambi hizo na kuanzisha ushirikiano wan chi zisizofungamana na upande wowote.



Mataifa masikini, yamekuwa yakijaribu kutafuta uhuru wake wa kisiasa na kiuchumi kwa njia ya amani na utulivu, lakini yamekuwa yakiwekewa vikwazo vingi kutoka katika mataifa yale yaliyoendelea kiuchumi na kisiasa hata kufanyiwa maamuzi ambayo pengine yamediriki hata kwenda kinyume na Haki za Binadamu.



Nchi hizi (masikini) zimekuwa zikikosa msimamo wao thabiti na hata kubanwa kwa kila njia katika Nyanja za uchumi na siasa kwa kufanyiwa maamuzi. Kwa mfano kila tunachozalisha tunanauza kwa bei ya kupangiwa na ambayo ni ya chini sana katika soko la kimataifa na kila tunachonunua kikiwa ni cha bei Ghali. Kwa maana hiyo basi naweza sema kuwa Jitihada zote za nchi masikini za kutaka kujikomboa na kujitafutia maendeleo zinaonekana kuwa ni kazi bure kama hatutaweza kujitegemea na kuzidi kuzihusudu na kuzitegemea nchi tajiri zitusaidie katika kilio chetu cha kujiokomboa bila sisi wenyewe kuwa na mipango madhubuti na kuifanyia kazi.



Nchi changa hazina budi kuanzisha mikakati mbalimbali itakayowezesha kujikomboa kikamilifu. Kwa mfano uanzishwaji wa umoja wa soko nafuu wa bidhaa zetu, uimarishwaji wa njia za mawasiliano na uchukuzi, ulinzi wa pamoja hayo ni baadhi tu ya mbinu zinazoweza kusaidia katika kuleta ukombozi katika mataifa masikini.



Viongozi nao hawana budi kuungana kwa kauli na vitendo. Hakuna sababu ya kuyaogopa mataifa makubwa kiuchumi kwani kitendo hicho ndicho kinayafanya mataifa mengi Masikini kuwa vibaraka wa mataifa hayo.



Hivyo basi, Mataifa masikini kokote Duniani hatuna budi kuungana kwa hali na mali hadi tone la mwisholimekombolewa kutoka kwenye uonevu, mateso na kunyanyaswa na mataifa haya makubwa kiuchumi kwani

“MBINU ZA KUJIKOMBOA ZINAPATIKANA KWENYE UWANJA WA UKOMBOZI (MAPAMBANO)”.

Mapambano yakiendelea ushindi ni lazima.

Thursday, 13 October 2011

HIVI NDIVYO SIKU YA PAULINA ILIKUWA

Mambo yakaanza hivi.
Tukiwa twamalizia siku hii ya leo siku iliyokuwa "maalyumu" kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtoto Paulina Arriana Bandio nipende kutoa shukrani kwa woote mlioshiriki nasi kwa namna moja ama nyingine kuiwezesha siku hii kufana kwa kiasi ilichofana.
Hongera Saana Mjukuu wetu. We are so Proud of You.
Hakika imefana hasa kwa sababu ameweza sherehekea sherehe hii akiwa na Mama, Babu, Bibi na Baba wadogo zake (Kakulu na Kato) Na pia kuweza jumuika na baadhi ya watoto wenzake katika sherehe hii.
Twaamini hii itakuwa kumbukumbu nzuri sana sio leo tu bali maishani mwake mwoote. Nasi twazidi muombea Baraka nyingi, Hekima, Upendo na Moyo wa huruma bila ya kusahau kumcha Mwenyezi Mungu aliye Muweza wa yoote.
Matukio mengine kwa ufupi ni kama yaonekanavyo hapo chini;
Wa kwanza nilishazima sasa ni zamu ya huu tena,
Hayaaaaaaa. Nazimaaaaa.
Wooow! I thank God I have made it, 
This is a special Cake for you BABU.
Asanteeeeee na Hongera sana mjukuu wa Jina.
This is for You Mummy. I love you so much.

Na hawa ndio Maswahiba wangu huku.
Asanteni nyote kwa kuwa nasi kwa namna moja ama nyingine katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto Paulina.
BARIKIWA.

HAPPY BIRTHDAY SUPER PAULINA.


The Little Angle (Napenda sana kumuita MAMA)
Ni jambo la pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukulinda hadi leo hii uadhimishapo miaka miwili tangu kuzaliwa kwako. Hakika ni safari ndefu ila twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake na hata kuweza fikia hapa.

Pia nitumie fursa hii kipekee kuwakaribisha sana Nyumbani Bukoba Tanzania Wewe (PAU) na Mama Pia.
Mama na Mwana. Karibuni Sana Bukoba wapendwa.
Twafurahi sana kujumuika nanyi katika sherehe hii na kuwa nanyi katika kipindi chote tutachobahatika kuwa nanyi.
 Hakika ni furaha sana kwetu sisi kama Familia na hata kwa kila mmoja wetu kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda safarini mpaka kuwafikisha salama na pia kuwashukuru ninyi kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali hadi kufikia Azma yenu ya kufika huku. Ujio wenu ni ishara tosha ya upendo wenu kwetu na si twaahidi kushirikiana nanyi katika kipindi chote tutachokuwa nanyi.
The Super Parents with their Angel P.A.B
Hivyo basi twawapenda na kuwaombea muwe na Afya tele na amani kwa kipindi chote tutakachokuwa nanyi huku tukimwombea pia kaka yetu Mubelwa (Baba Pau) azidishiwe afya njema na Baraka kwa kipindi choote tutakachokuwa nanyi na hata baada ya Hapo.

KARIBUNI SANA TANZANIA,

KARIBUNI SANA BUKOBA  MAMA PAULINA  NA PAULINA. 

Na mwisho niseme
HAPPY BIRTHDAY Pauliana Arianna Bandio. 

BARAKA KWENU NYOOTE.

Friday, 23 September 2011

HAPPY BELATED EARTH DAY ANNA

Hii ndio zawadi yako Rafiki yangu.

Ni siku nyingine ambayo ni ya muhimu sana pengine kuliko hata siku yoyote kwa maana ndiyo siku wakumbuka siku yako ya Kuzaliwa. Ni wazi kuwa LEO unaongeza mwaka mwingine mmoja ambao ni hatua muhimu sana katika maisha yetu wanadamu na ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema mengi aliyokutendea na kukuepusha hadi kufikia tena siku hii ya leo. Pia kuwashukuru na kuwapongeza sana wazazi kwa malezi Bora waliyokupa hadi sasa kwani wao kama nguzo ya familia wamekuwa na mchango mkubwa kwako kukufanya uwe ANNA yule ambaye jamii tunamuona sasa.
Mtoto mzaliwa Anna Tecla

Katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Kwako nami nimewiwa nikutakie maisha mengine mema yenye furaha na upendo. Uzidi kudumu katika Upendo na kuishi vyema na watu. Hivyo basi nipende kusema “celebrate hundreds of such birthdays in the coming time with happiness and joy.”
HAPPY BELATED EARTH DAY BEST FRIEND.

Thursday, 22 September 2011

SALAMU ZA MMISO KWENU WAPENDWA.

Baadhi ya Group mates wangu.
Remember that "when you ask and receive what you have asked the prayer is not complete until you have given thanks."
Nipende kitumia  nafasi hii kuwashukuru wapendwa wangu hawa kwa jinsi tumekuwa wote katika shughuli nzima za masomo. Kiukweli nimepata jifunza mengi kutoka kwenu na hata kwa wengine ila kwa muda mrefu sana nimekuwa nanyi na tumejumuika pamoja katika shughuli nyingi za kielimu, kiuchumi na hata kijamii.
Best Friend Silvester.
I real enjoyed mpaka sasa nawaza kama nitajapata watu wa kushirikiana kiukaribu na kuwa wote kama ndugu mithili ya vile tulivyokuwa twaishi wote chuo. 
Baadhi ya wandugu katika matukio
Ninaamini bado kuna  mengi sana nilitakiwa jifunza kutoka kwa kila mmoja wenu na hata kwa ujumla wenu ila kwa ajili ya muda haikuwezekana ila kwa kipindi cha miaka mitatu tumekuwa wote sina budi kujivunia mchango wangu kwenu na hata kukiri kuwa ninawamis sana. 
L-R. Twin, Brother Fortunatus and I.
Hata hivyo ninawatakia kila lililo jema na kuwaombea uzima na afya ili kutimiza malengo yenu.
NINAWAMIS, NAWAPENDA, NAWAOMBEA NA NAWATAKIA MAISHA MEMA.
BLESSINGS TO YOU ALL.