Friday, 16 September 2011

HONGERA ALEENA KWA KUKUMBUKA SIKU YAKO YA KUZALIWA

Kati ya sikukuu za binafsi kuna siku za kukumbuka matukio ya pekee kama tarehe ya kuzaliwa, Siku ya kuzaliwa, moja ya matukio ya sherehe duniani
Leo ni siku ya kuzaliwa kwako Uncle  Aleena Faraja, na hivyo basi twajumuika nawe katika kusherehekea kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa na kutimiza mwaka MMOJA (1). Ni siku kama hii ndiyo ulifanikiwa kuona jua kuvuta pumzi kwa mara ya kwanza. Ni siku yenye thamani  na maana kubwa sana kwako.
Kipekee twawapongeza pia wazazi, ndugu na jamaa wote kwa support walioonyesha katika juhudi za malezi yako kwa kipindi chote tokea kuzaliwa kwako na twawaombea wazidi kuwa waaminifu na waalimu wako wazuri katika kukukuza kiroho kimwili na kiakili.
Utamueleza nini Dada Kapwingo

Katika kukumbuka
 siku hii, twanapenda,  kukutakia maisha marefu sana yaliyojaa furaha, amani na mafanikio. Amani ya Bwana ipitayo fahamu zote ikuangazie, ubarikiwe na kufanikiwa  katika maisha yako nasi tuko nyuma yako kuhakikisha watimiza mema yote utakayokuwa nayo katika maisha yako yote.

Uwe na wakati mzuri daima na Mwenyezi Mungu akujaalie maisha marefu zaidi yenye furaha, amani, na mafanikio tele. Na zaidi, akupe nafasi ya kusherehekea siku nyingi zaidi kama ya leo.

HAPPY EARTH DAY ALEENA FARAJA.

2 comments:

  1. Hongera sana kwa siku ya kuzaliwa kwako Aleena Faraja. Mwenyezi Mungu uzidi kuwapa nguvu wazazi ili waweze kumlea na kumpa mtoto huyu maisha mema na yenye baraka.HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA.

    ReplyDelete
  2. I'm very much humbled with ur comments dada Yasinta. May the Almighty God Bless you pia.

    ReplyDelete