Thursday, 13 October 2011

HIVI NDIVYO SIKU YA PAULINA ILIKUWA

Mambo yakaanza hivi.
Tukiwa twamalizia siku hii ya leo siku iliyokuwa "maalyumu" kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtoto Paulina Arriana Bandio nipende kutoa shukrani kwa woote mlioshiriki nasi kwa namna moja ama nyingine kuiwezesha siku hii kufana kwa kiasi ilichofana.
Hongera Saana Mjukuu wetu. We are so Proud of You.
Hakika imefana hasa kwa sababu ameweza sherehekea sherehe hii akiwa na Mama, Babu, Bibi na Baba wadogo zake (Kakulu na Kato) Na pia kuweza jumuika na baadhi ya watoto wenzake katika sherehe hii.
Twaamini hii itakuwa kumbukumbu nzuri sana sio leo tu bali maishani mwake mwoote. Nasi twazidi muombea Baraka nyingi, Hekima, Upendo na Moyo wa huruma bila ya kusahau kumcha Mwenyezi Mungu aliye Muweza wa yoote.
Matukio mengine kwa ufupi ni kama yaonekanavyo hapo chini;
Wa kwanza nilishazima sasa ni zamu ya huu tena,
Hayaaaaaaa. Nazimaaaaa.
Wooow! I thank God I have made it, 
This is a special Cake for you BABU.
Asanteeeeee na Hongera sana mjukuu wa Jina.
This is for You Mummy. I love you so much.

Na hawa ndio Maswahiba wangu huku.
Asanteni nyote kwa kuwa nasi kwa namna moja ama nyingine katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto Paulina.
BARIKIWA.

HAPPY BIRTHDAY SUPER PAULINA.


The Little Angle (Napenda sana kumuita MAMA)
Ni jambo la pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukulinda hadi leo hii uadhimishapo miaka miwili tangu kuzaliwa kwako. Hakika ni safari ndefu ila twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake na hata kuweza fikia hapa.

Pia nitumie fursa hii kipekee kuwakaribisha sana Nyumbani Bukoba Tanzania Wewe (PAU) na Mama Pia.
Mama na Mwana. Karibuni Sana Bukoba wapendwa.
Twafurahi sana kujumuika nanyi katika sherehe hii na kuwa nanyi katika kipindi chote tutachobahatika kuwa nanyi.
 Hakika ni furaha sana kwetu sisi kama Familia na hata kwa kila mmoja wetu kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda safarini mpaka kuwafikisha salama na pia kuwashukuru ninyi kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali hadi kufikia Azma yenu ya kufika huku. Ujio wenu ni ishara tosha ya upendo wenu kwetu na si twaahidi kushirikiana nanyi katika kipindi chote tutachokuwa nanyi.
The Super Parents with their Angel P.A.B
Hivyo basi twawapenda na kuwaombea muwe na Afya tele na amani kwa kipindi chote tutakachokuwa nanyi huku tukimwombea pia kaka yetu Mubelwa (Baba Pau) azidishiwe afya njema na Baraka kwa kipindi choote tutakachokuwa nanyi na hata baada ya Hapo.

KARIBUNI SANA TANZANIA,

KARIBUNI SANA BUKOBA  MAMA PAULINA  NA PAULINA. 

Na mwisho niseme
HAPPY BIRTHDAY Pauliana Arianna Bandio. 

BARAKA KWENU NYOOTE.

Friday, 23 September 2011

HAPPY BELATED EARTH DAY ANNA

Hii ndio zawadi yako Rafiki yangu.

Ni siku nyingine ambayo ni ya muhimu sana pengine kuliko hata siku yoyote kwa maana ndiyo siku wakumbuka siku yako ya Kuzaliwa. Ni wazi kuwa LEO unaongeza mwaka mwingine mmoja ambao ni hatua muhimu sana katika maisha yetu wanadamu na ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema mengi aliyokutendea na kukuepusha hadi kufikia tena siku hii ya leo. Pia kuwashukuru na kuwapongeza sana wazazi kwa malezi Bora waliyokupa hadi sasa kwani wao kama nguzo ya familia wamekuwa na mchango mkubwa kwako kukufanya uwe ANNA yule ambaye jamii tunamuona sasa.
Mtoto mzaliwa Anna Tecla

Katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Kwako nami nimewiwa nikutakie maisha mengine mema yenye furaha na upendo. Uzidi kudumu katika Upendo na kuishi vyema na watu. Hivyo basi nipende kusema “celebrate hundreds of such birthdays in the coming time with happiness and joy.”
HAPPY BELATED EARTH DAY BEST FRIEND.

Thursday, 22 September 2011

SALAMU ZA MMISO KWENU WAPENDWA.

Baadhi ya Group mates wangu.
Remember that "when you ask and receive what you have asked the prayer is not complete until you have given thanks."
Nipende kitumia  nafasi hii kuwashukuru wapendwa wangu hawa kwa jinsi tumekuwa wote katika shughuli nzima za masomo. Kiukweli nimepata jifunza mengi kutoka kwenu na hata kwa wengine ila kwa muda mrefu sana nimekuwa nanyi na tumejumuika pamoja katika shughuli nyingi za kielimu, kiuchumi na hata kijamii.
Best Friend Silvester.
I real enjoyed mpaka sasa nawaza kama nitajapata watu wa kushirikiana kiukaribu na kuwa wote kama ndugu mithili ya vile tulivyokuwa twaishi wote chuo. 
Baadhi ya wandugu katika matukio
Ninaamini bado kuna  mengi sana nilitakiwa jifunza kutoka kwa kila mmoja wenu na hata kwa ujumla wenu ila kwa ajili ya muda haikuwezekana ila kwa kipindi cha miaka mitatu tumekuwa wote sina budi kujivunia mchango wangu kwenu na hata kukiri kuwa ninawamis sana. 
L-R. Twin, Brother Fortunatus and I.
Hata hivyo ninawatakia kila lililo jema na kuwaombea uzima na afya ili kutimiza malengo yenu.
NINAWAMIS, NAWAPENDA, NAWAOMBEA NA NAWATAKIA MAISHA MEMA.
BLESSINGS TO YOU ALL.

Monday, 19 September 2011

UJIO WA VYUO VIKUU BUKOBA NINI FAIDA NA HASARA ZAKE KWETU?

Hii ni sehemu ndogo tu ya mji wa Bukoba.
Ujio wa vyuo vikuu katika mji wa Bukoba ambayo ni makao makuu ya mkoa wa Kagera ni moja ya mambo ambayo ninayaona kuwa ya kimaendeleo na changamoto katika mkoa huu hasa Bukoba Mjini. Kwa kipindi kirefu sasa mkoa huu umekuwa nyuma kimaendeleo japo wasemekana kuwa hazina ya wasomi na mali asili nyingi ambazo kama hivi vingetumika kiufasaha basi usingekuwa hapa ulipo sasa kimaendeleo.

Lakini hasa ninachotaka kuangalia zaidi katika suala zima la ujio wa vyuo vikuu ni suala zima la "ni nini faida na hasara za ujio wa vyuo hivi" na ni jinsi gani twaweza punguza madhara na kutafuta manufaa zaidi katika ujio huo.
Katika siku za hivi karibuni twatumainia NDAKI YA MTAKATIFU AGUSTINO TANZANIA (St. Augustine University of Tanzania) wafungue tawi lao kilipokuwa chuo cha ualimu St. Francis Nkindo nje kidogo ya mji wa Bukoba. Wakati huo huo bado maandalizi ya Ndaki ya Tumaini itakayoitwa Josiah Kibira University Collage (JOKUCo) yakiwa kwenye hatua za mwisho.
Nilipata sikia Askofu Nestory Timanywa na Msaidizi wake Askofu Methodius Kilaini wamekwenda elimisha watu Dar es Salaam kuhusu chuo kinachoanza Bukoba. nilishangaa sana,  nikajiuliza watakaonufaika zaidi na chuo hiki ni watu wa dar ama wa Bukoba? je ni elimu gani wametoa kwa wana Bukoba ili kujihadhari na yatakayotokea kulingana na ufunguzi wa vyuo hivi? Ni vema sasa wananchi wakajua ni nini faida na madhara ya uwepo wa vyuo vikuu katika maeneo yao ili kuwawezesha kujua ni nini wafanye katika kijikinga dhidi madhara yake na kujipanga zaidi katika kujua wananufaika vipi na ujio wake.
Ni suala lililo wazi kuwa uwepo wa vyuo vikuu mjini Bukoba utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha elimu kwa wakazi wa mji huu, kodi za mapato kwa sekta husika, Ajira na Kukua kwa uchumi wa wananchi na mji kwa ujumla.

Hata hivyo ujio wa vyuo hivi pia utakuwa na hasara zake kama kuchangia migogoro ya ardhi, biashara, ongezeko la matukio ya kihalifu, mfumuko wa bei katika bidhaa zinazopatikana humu mjini, kutokana na misuguano ya wenye pesa na madaraka kutaka kuwanyonya wale wasionacho na baadhi ya watu kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanavyuo hivyo kuleta ongezeko la maambukizi ya magonjwa kama VVU/UKIMWI na magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni, ndoa kuvunjika na ongezeko la watoto wa mitaani katika mji wa Bukoba.
Swali kubwa ambalo bado najiuliza ni  Je, Halmashauri ya Manispaa ya wilaya hii hasa kwa eneo la mji huu wamejipanga kwa kiasi gani katika kukabiliana na matatizo haya na kujiimarisha katika mipago miji ili mji usizidi kutokuwa na mipango na kuwa na vichochoro vingi vya kuongeza matukio ya uhalifu na hofu ya Raia wa kawaida na wanachuo kwa ujumla?

Pengine kati ya mambo nawaza ni kuweza saidia wazazi na wanandoa kwa kuwashauri kukaa na watoto wao na kuwaeleza namna wanavyoweza kujilinda dhidi ya vishawishi vinavyotolewa na wanafunzi. Na hii ianzie kwenye ngazi ya familia ili kuwia rahisi hata watoto kuelewa.

Pia kutoa ushauri kwa Jeshi la polisi kuweka vituo vya polisi karibia na maeneo ya chuo kwa ajili ya kulinda mali za chuo, wanachuo na raia ambao wanategemea kuweka miradi itakayowanufaisha kwa ujio wa vyuo hivi itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi wakati huo wakivisaidia vyuo na wanachuo kujipatia mahitaji yao kwa karibu. Kwa maana hiyo basi Jeshi letu liwe makini sana katika ulinzi likisaidiana na wananchi katika kuleta maendeleo na sio kwenda kinyume na hayo kwani Jeshi hili limepewa dhamana ya kutulinda na sio kutuwinda.

Natumai kama haya yatatekelezwa na mengine mengi ambayo sikuweza yataja basi tutatarajia kuwa na maendeleo chanya yatokanayo na ujio wa vyuo katika mji wetu na kuvutia wawekezaji na wageni wengi kufika huku.
NAWATAKIENI KILA LAKHERI KATIKA KUFANIKISHA MIPANGO YOTE HII.