Friday 2 December 2011

UKWELI UKO WAPI?

Labda kwa vile nimo ndani ya moja ya nchi masikini kiuchumi hivyo naweza shindwa onyesha wazi ulipo ukweli juu ya maendeleo ya nchi hizi masikini Duniani.
Tokea kuwako kwa Kambi mbili zenye nguvu na zinazokinzana Duniani kambi ya mfumo wa nchi za kibepari na Kambi ya mfumo wa nchi za Kijamaa, kumekuwako na maonevu na unyonyaji mwingi sana dhidi ya nchi zinazoendelea ufanywao na mataifa makubwa na yenye nguvu kiuchumi.



Mgawanyiko wa kambi hizi mbili ulikuwako tokea mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 lakini ukaja kukua baada ya Vita vikuu vya pili vya Dunia ambapo kambi hizi mbili zilizidi pingana kiitikadi na kijeshi.

Kambi ya Kibepari iliongozwa na Marekani na kambi wa Kijamaa iliongozwa na Urusi. Katika kambi hizi, mataifa masikini yaliingizwa kwenye mikataba ya kujiunga na kambi moja wapo japo baadhi ya mataifa yalikataa kujiunga na kambi hizo na kuanzisha ushirikiano wan chi zisizofungamana na upande wowote.



Mataifa masikini, yamekuwa yakijaribu kutafuta uhuru wake wa kisiasa na kiuchumi kwa njia ya amani na utulivu, lakini yamekuwa yakiwekewa vikwazo vingi kutoka katika mataifa yale yaliyoendelea kiuchumi na kisiasa hata kufanyiwa maamuzi ambayo pengine yamediriki hata kwenda kinyume na Haki za Binadamu.



Nchi hizi (masikini) zimekuwa zikikosa msimamo wao thabiti na hata kubanwa kwa kila njia katika Nyanja za uchumi na siasa kwa kufanyiwa maamuzi. Kwa mfano kila tunachozalisha tunanauza kwa bei ya kupangiwa na ambayo ni ya chini sana katika soko la kimataifa na kila tunachonunua kikiwa ni cha bei Ghali. Kwa maana hiyo basi naweza sema kuwa Jitihada zote za nchi masikini za kutaka kujikomboa na kujitafutia maendeleo zinaonekana kuwa ni kazi bure kama hatutaweza kujitegemea na kuzidi kuzihusudu na kuzitegemea nchi tajiri zitusaidie katika kilio chetu cha kujiokomboa bila sisi wenyewe kuwa na mipango madhubuti na kuifanyia kazi.



Nchi changa hazina budi kuanzisha mikakati mbalimbali itakayowezesha kujikomboa kikamilifu. Kwa mfano uanzishwaji wa umoja wa soko nafuu wa bidhaa zetu, uimarishwaji wa njia za mawasiliano na uchukuzi, ulinzi wa pamoja hayo ni baadhi tu ya mbinu zinazoweza kusaidia katika kuleta ukombozi katika mataifa masikini.



Viongozi nao hawana budi kuungana kwa kauli na vitendo. Hakuna sababu ya kuyaogopa mataifa makubwa kiuchumi kwani kitendo hicho ndicho kinayafanya mataifa mengi Masikini kuwa vibaraka wa mataifa hayo.



Hivyo basi, Mataifa masikini kokote Duniani hatuna budi kuungana kwa hali na mali hadi tone la mwisholimekombolewa kutoka kwenye uonevu, mateso na kunyanyaswa na mataifa haya makubwa kiuchumi kwani

“MBINU ZA KUJIKOMBOA ZINAPATIKANA KWENYE UWANJA WA UKOMBOZI (MAPAMBANO)”.

Mapambano yakiendelea ushindi ni lazima.

Thursday 13 October 2011

HIVI NDIVYO SIKU YA PAULINA ILIKUWA

Mambo yakaanza hivi.
Tukiwa twamalizia siku hii ya leo siku iliyokuwa "maalyumu" kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtoto Paulina Arriana Bandio nipende kutoa shukrani kwa woote mlioshiriki nasi kwa namna moja ama nyingine kuiwezesha siku hii kufana kwa kiasi ilichofana.
Hongera Saana Mjukuu wetu. We are so Proud of You.
Hakika imefana hasa kwa sababu ameweza sherehekea sherehe hii akiwa na Mama, Babu, Bibi na Baba wadogo zake (Kakulu na Kato) Na pia kuweza jumuika na baadhi ya watoto wenzake katika sherehe hii.
Twaamini hii itakuwa kumbukumbu nzuri sana sio leo tu bali maishani mwake mwoote. Nasi twazidi muombea Baraka nyingi, Hekima, Upendo na Moyo wa huruma bila ya kusahau kumcha Mwenyezi Mungu aliye Muweza wa yoote.
Matukio mengine kwa ufupi ni kama yaonekanavyo hapo chini;
Wa kwanza nilishazima sasa ni zamu ya huu tena,
Hayaaaaaaa. Nazimaaaaa.
Wooow! I thank God I have made it, 
This is a special Cake for you BABU.
Asanteeeeee na Hongera sana mjukuu wa Jina.
This is for You Mummy. I love you so much.

Na hawa ndio Maswahiba wangu huku.
Asanteni nyote kwa kuwa nasi kwa namna moja ama nyingine katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto Paulina.
BARIKIWA.

HAPPY BIRTHDAY SUPER PAULINA.


The Little Angle (Napenda sana kumuita MAMA)
Ni jambo la pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukulinda hadi leo hii uadhimishapo miaka miwili tangu kuzaliwa kwako. Hakika ni safari ndefu ila twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake na hata kuweza fikia hapa.

Pia nitumie fursa hii kipekee kuwakaribisha sana Nyumbani Bukoba Tanzania Wewe (PAU) na Mama Pia.
Mama na Mwana. Karibuni Sana Bukoba wapendwa.
Twafurahi sana kujumuika nanyi katika sherehe hii na kuwa nanyi katika kipindi chote tutachobahatika kuwa nanyi.
 Hakika ni furaha sana kwetu sisi kama Familia na hata kwa kila mmoja wetu kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda safarini mpaka kuwafikisha salama na pia kuwashukuru ninyi kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali hadi kufikia Azma yenu ya kufika huku. Ujio wenu ni ishara tosha ya upendo wenu kwetu na si twaahidi kushirikiana nanyi katika kipindi chote tutachokuwa nanyi.
The Super Parents with their Angel P.A.B
Hivyo basi twawapenda na kuwaombea muwe na Afya tele na amani kwa kipindi chote tutakachokuwa nanyi huku tukimwombea pia kaka yetu Mubelwa (Baba Pau) azidishiwe afya njema na Baraka kwa kipindi choote tutakachokuwa nanyi na hata baada ya Hapo.

KARIBUNI SANA TANZANIA,

KARIBUNI SANA BUKOBA  MAMA PAULINA  NA PAULINA. 

Na mwisho niseme
HAPPY BIRTHDAY Pauliana Arianna Bandio. 

BARAKA KWENU NYOOTE.

Friday 23 September 2011

HAPPY BELATED EARTH DAY ANNA

Hii ndio zawadi yako Rafiki yangu.

Ni siku nyingine ambayo ni ya muhimu sana pengine kuliko hata siku yoyote kwa maana ndiyo siku wakumbuka siku yako ya Kuzaliwa. Ni wazi kuwa LEO unaongeza mwaka mwingine mmoja ambao ni hatua muhimu sana katika maisha yetu wanadamu na ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema mengi aliyokutendea na kukuepusha hadi kufikia tena siku hii ya leo. Pia kuwashukuru na kuwapongeza sana wazazi kwa malezi Bora waliyokupa hadi sasa kwani wao kama nguzo ya familia wamekuwa na mchango mkubwa kwako kukufanya uwe ANNA yule ambaye jamii tunamuona sasa.
Mtoto mzaliwa Anna Tecla

Katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Kwako nami nimewiwa nikutakie maisha mengine mema yenye furaha na upendo. Uzidi kudumu katika Upendo na kuishi vyema na watu. Hivyo basi nipende kusema “celebrate hundreds of such birthdays in the coming time with happiness and joy.”
HAPPY BELATED EARTH DAY BEST FRIEND.

Thursday 22 September 2011

SALAMU ZA MMISO KWENU WAPENDWA.

Baadhi ya Group mates wangu.
Remember that "when you ask and receive what you have asked the prayer is not complete until you have given thanks."
Nipende kitumia  nafasi hii kuwashukuru wapendwa wangu hawa kwa jinsi tumekuwa wote katika shughuli nzima za masomo. Kiukweli nimepata jifunza mengi kutoka kwenu na hata kwa wengine ila kwa muda mrefu sana nimekuwa nanyi na tumejumuika pamoja katika shughuli nyingi za kielimu, kiuchumi na hata kijamii.
Best Friend Silvester.
I real enjoyed mpaka sasa nawaza kama nitajapata watu wa kushirikiana kiukaribu na kuwa wote kama ndugu mithili ya vile tulivyokuwa twaishi wote chuo. 
Baadhi ya wandugu katika matukio
Ninaamini bado kuna  mengi sana nilitakiwa jifunza kutoka kwa kila mmoja wenu na hata kwa ujumla wenu ila kwa ajili ya muda haikuwezekana ila kwa kipindi cha miaka mitatu tumekuwa wote sina budi kujivunia mchango wangu kwenu na hata kukiri kuwa ninawamis sana. 
L-R. Twin, Brother Fortunatus and I.
Hata hivyo ninawatakia kila lililo jema na kuwaombea uzima na afya ili kutimiza malengo yenu.
NINAWAMIS, NAWAPENDA, NAWAOMBEA NA NAWATAKIA MAISHA MEMA.
BLESSINGS TO YOU ALL.

Monday 19 September 2011

UJIO WA VYUO VIKUU BUKOBA NINI FAIDA NA HASARA ZAKE KWETU?

Hii ni sehemu ndogo tu ya mji wa Bukoba.
Ujio wa vyuo vikuu katika mji wa Bukoba ambayo ni makao makuu ya mkoa wa Kagera ni moja ya mambo ambayo ninayaona kuwa ya kimaendeleo na changamoto katika mkoa huu hasa Bukoba Mjini. Kwa kipindi kirefu sasa mkoa huu umekuwa nyuma kimaendeleo japo wasemekana kuwa hazina ya wasomi na mali asili nyingi ambazo kama hivi vingetumika kiufasaha basi usingekuwa hapa ulipo sasa kimaendeleo.

Lakini hasa ninachotaka kuangalia zaidi katika suala zima la ujio wa vyuo vikuu ni suala zima la "ni nini faida na hasara za ujio wa vyuo hivi" na ni jinsi gani twaweza punguza madhara na kutafuta manufaa zaidi katika ujio huo.
Katika siku za hivi karibuni twatumainia NDAKI YA MTAKATIFU AGUSTINO TANZANIA (St. Augustine University of Tanzania) wafungue tawi lao kilipokuwa chuo cha ualimu St. Francis Nkindo nje kidogo ya mji wa Bukoba. Wakati huo huo bado maandalizi ya Ndaki ya Tumaini itakayoitwa Josiah Kibira University Collage (JOKUCo) yakiwa kwenye hatua za mwisho.
Nilipata sikia Askofu Nestory Timanywa na Msaidizi wake Askofu Methodius Kilaini wamekwenda elimisha watu Dar es Salaam kuhusu chuo kinachoanza Bukoba. nilishangaa sana,  nikajiuliza watakaonufaika zaidi na chuo hiki ni watu wa dar ama wa Bukoba? je ni elimu gani wametoa kwa wana Bukoba ili kujihadhari na yatakayotokea kulingana na ufunguzi wa vyuo hivi? Ni vema sasa wananchi wakajua ni nini faida na madhara ya uwepo wa vyuo vikuu katika maeneo yao ili kuwawezesha kujua ni nini wafanye katika kijikinga dhidi madhara yake na kujipanga zaidi katika kujua wananufaika vipi na ujio wake.
Ni suala lililo wazi kuwa uwepo wa vyuo vikuu mjini Bukoba utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha elimu kwa wakazi wa mji huu, kodi za mapato kwa sekta husika, Ajira na Kukua kwa uchumi wa wananchi na mji kwa ujumla.

Hata hivyo ujio wa vyuo hivi pia utakuwa na hasara zake kama kuchangia migogoro ya ardhi, biashara, ongezeko la matukio ya kihalifu, mfumuko wa bei katika bidhaa zinazopatikana humu mjini, kutokana na misuguano ya wenye pesa na madaraka kutaka kuwanyonya wale wasionacho na baadhi ya watu kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanavyuo hivyo kuleta ongezeko la maambukizi ya magonjwa kama VVU/UKIMWI na magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni, ndoa kuvunjika na ongezeko la watoto wa mitaani katika mji wa Bukoba.
Swali kubwa ambalo bado najiuliza ni  Je, Halmashauri ya Manispaa ya wilaya hii hasa kwa eneo la mji huu wamejipanga kwa kiasi gani katika kukabiliana na matatizo haya na kujiimarisha katika mipago miji ili mji usizidi kutokuwa na mipango na kuwa na vichochoro vingi vya kuongeza matukio ya uhalifu na hofu ya Raia wa kawaida na wanachuo kwa ujumla?

Pengine kati ya mambo nawaza ni kuweza saidia wazazi na wanandoa kwa kuwashauri kukaa na watoto wao na kuwaeleza namna wanavyoweza kujilinda dhidi ya vishawishi vinavyotolewa na wanafunzi. Na hii ianzie kwenye ngazi ya familia ili kuwia rahisi hata watoto kuelewa.

Pia kutoa ushauri kwa Jeshi la polisi kuweka vituo vya polisi karibia na maeneo ya chuo kwa ajili ya kulinda mali za chuo, wanachuo na raia ambao wanategemea kuweka miradi itakayowanufaisha kwa ujio wa vyuo hivi itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi wakati huo wakivisaidia vyuo na wanachuo kujipatia mahitaji yao kwa karibu. Kwa maana hiyo basi Jeshi letu liwe makini sana katika ulinzi likisaidiana na wananchi katika kuleta maendeleo na sio kwenda kinyume na hayo kwani Jeshi hili limepewa dhamana ya kutulinda na sio kutuwinda.

Natumai kama haya yatatekelezwa na mengine mengi ambayo sikuweza yataja basi tutatarajia kuwa na maendeleo chanya yatokanayo na ujio wa vyuo katika mji wetu na kuvutia wawekezaji na wageni wengi kufika huku.
NAWATAKIENI KILA LAKHERI KATIKA KUFANIKISHA MIPANGO YOTE HII.

Friday 16 September 2011

HONGERA ALEENA KWA KUKUMBUKA SIKU YAKO YA KUZALIWA

Kati ya sikukuu za binafsi kuna siku za kukumbuka matukio ya pekee kama tarehe ya kuzaliwa, Siku ya kuzaliwa, moja ya matukio ya sherehe duniani
Leo ni siku ya kuzaliwa kwako Uncle  Aleena Faraja, na hivyo basi twajumuika nawe katika kusherehekea kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa na kutimiza mwaka MMOJA (1). Ni siku kama hii ndiyo ulifanikiwa kuona jua kuvuta pumzi kwa mara ya kwanza. Ni siku yenye thamani  na maana kubwa sana kwako.
Kipekee twawapongeza pia wazazi, ndugu na jamaa wote kwa support walioonyesha katika juhudi za malezi yako kwa kipindi chote tokea kuzaliwa kwako na twawaombea wazidi kuwa waaminifu na waalimu wako wazuri katika kukukuza kiroho kimwili na kiakili.
Utamueleza nini Dada Kapwingo

Katika kukumbuka
 siku hii, twanapenda,  kukutakia maisha marefu sana yaliyojaa furaha, amani na mafanikio. Amani ya Bwana ipitayo fahamu zote ikuangazie, ubarikiwe na kufanikiwa  katika maisha yako nasi tuko nyuma yako kuhakikisha watimiza mema yote utakayokuwa nayo katika maisha yako yote.

Uwe na wakati mzuri daima na Mwenyezi Mungu akujaalie maisha marefu zaidi yenye furaha, amani, na mafanikio tele. Na zaidi, akupe nafasi ya kusherehekea siku nyingi zaidi kama ya leo.

HAPPY EARTH DAY ALEENA FARAJA.

Friday 11 February 2011

HAPPY BIRTHDATE BEST FRIEND RACHEL.



Rachel enzi Hizo.
Sijui ni lipi naweza kusema kueleza faraja niliyonayo kwa kufahamiana nawe. Najivunia mengi toka kwako. Kuanzia ukweli wa uwezo wako.Kuna kumbukumbu nyiingi maishani ambazo kwa wengine zaanza, na wengine zaendelea. Na hiyo ni sehemu ya siku yoyote ambayo kwa wengine ni "special"
Na leo ni siku muhimu kwa mmoja wa rafiki zangu aitwaye Rachel ambaye leo anatimiza mzunguko kamili wa mwaka maishani mwake. Ni "mwaka mpya" wa maisha yake na kama mmoja wa Best Friends , napenda kuungana naye katika siku hii muhimu kwake.
Akikumbuka moja ya siku yake ya kuzaliwa Udogoni.



Labda kwa kuwa nina tu-miaka kadhaa twa kukabiliana na maisha, nikuase kuwa maisha ya sasa ni ya kukabiliana na kile chema uaminicho. Kwa sasa wapo wengi ambao watajitahidi kuja na "wazo" hili ama lile kukufanya uamini kuwa HUWEZI KUFANYA UTAKALO NA KUWA UPENDAVYO.
Sikukuu ya kuzaliwa mwaka 2009.


Katika siku hii maalum kwako, nakutakia kila lililo jema katika miaka ijayo, nakupenda, nakuheshimu na nakuombea mafanikio.



HAPPY BIRTH DATE MAMA.

Thursday 10 February 2011

HIZI NI POLI-TRICKS.



Kaka yangu Mkubwa Mubelwa katika Blog yake anasegment  yake iitwayo "TANZANIA YANGU". Kiukweli naipenda sana na hujifunza na kucheka sana nionapo mambo ya kipuuzi yanayofanywa na Nchi yetu hasa kule BUNGENI. Siamini kama mambo serious yanaweza kujadiliwa kimasihara hivi ikiwa wabunge wamechaguliwa kuwawakilisha wanchi wa majimboni kwao.
Nilipokua nawaza kuandika kuhusu hilinakapata wazo kuwa ningesema TANZANIA YANGU INAYOMKANDA MBWA KIZAZI. Kwa nini nasema hivi? Wote twakumbuka dhahiri kuwa wakati Bunge likizinduliwa rasmi baada ya uchaguzi mkuu uliompatia ushindi Ndugu Jakaya M. Kikwete kuendelea kuongoza nchi kwa awamu ya pili na ya mwisho, Wabunge wa kambi kuu ya upinzani Bungeni (CHADEMA) walisusia kikao hicho na kuamua kutoka nje ya Bunge. Mengi yalisemwa na kuanza kusahaulika kama ilivyo kawaida ya Watanzania kusahau mapema ila kilichonisukuma hadi kuweka mawazo yangu kijiweni ni hali ya kushangaza ya Wabunge hao kukaa na kukubaliana na Hotuba ya Mh. Rais ilhali waliamua kutoka na kutoisikiliza. Kiukweli haikuniingia akilini na ndipo nikaanza amini kuwa Siasa sio mcheza mchafu ila wachezaji ndio wachafu. Kwa nini wawe wanafiki kiasi hicho sasa kama walijua watakuja kula matapishi yao? Na sasa nimegundua mbinu yao ya kugomea vikao na kutoka nje kisa wametofautiana kwa hoja na upinzani wenzao ama Chama tawala. Swali kwa hawa ndugu ni kwamba wanadhani kususa vikao na kutoka nje ni suluhisho la matatizo yao? Na wanawaza nini wakirudi majimboni na kuulizwa jinsi fani wamewawakilisha wananchi wao watajibu vp? Kwamba ni kwa kutoka kwenye vikao? Ila haya yote nayaona kama matokeo ya kuburuzwa kwa wanachama (wabunge) na Viongozi wa chama waliopo mjengoni na kuhamasisha migomo katika kutaka vuruga Amani wakijua wana watu wa kuwa support kutoka vyuoni. Na kama ndio njia za kushinikiza mabadiliko ya katiba kuwa ya haraka kama wanavyotaka naweza sema wataishia angukia pua kama tulivyoona vyama vya upinzani vilivyowahi kuleta upinzani kabla yao.

Tuesday 1 February 2011

SHULE ZA KATA

Picha kwa hisani ya Kaka FRANCIS GODWI












Ikiwa ni muda mchache umepita tokea matokeo ya shule za sekondari kutangazwa, twaweza pata picha halisi ya elimu bora iliyoahidi Serikali Tukufu. Siwezi sema moja kwa moja kuwa hii ndio kudhihirisha usemi wa "MWANZO MGUMU" maana huu nauona kuwa mwanzo wa mwisho. Serikali baada ya kujenga majengo wakishirikisha baadhi ya wananchi alifanikiwa kayajenga katika kila kata kama mpango maalumu wa kuendeleza elimu Tanzania na kupata sifa kedekede kutoka kwa wafadhili wake kama UNESCO. Kwa kiwango kikubwa japo bila ya kusikiliza ni nini wananchi wake wanataka, Serikali imekua ikijichukulia maamuzi na kuendelea kuwakumbatia hao iwaitao wafadhili na kusahau kuwa "MTEGEMEA CHA NDUGUYE, HUFA MASIKINI."Kiukweli tunashindwa fanya maendeleo yetu kwa kuwa twadhani hao tunaowakumbatia NDIO WENYE MAJIBU SAHIHI YA MATATIZO YETU na kuwa wanania njema nasi lakini mimi nazidi amini bila sisi kujikana hatufiki kokote. Tuachane na Hayo, Takribani miaka minne iliyopita, Shule nyingi za kata al maarufu kama YEBOYEBO zilifunguliwa kwa nia Nzuri tu ya kutoa elimu kwa Watanzania ila sasa matokeo yametoka ni AIBU. hii ni kwa kuwa serikali ilijiandaa kutengeneza majengo wakidhani ndio maana halisi ya Shule, mengi ya majengo hayo hayakuwa na vifaa vya kufundishia wala waalimu hali iliyowalazimu hata wale walioteuliwa kwenda kwenye hizo shule kugoma. Sijui ila nipende tu pia naweza sema hili ya kuwa udhaifu ulioonekana ndio nahisi ulitumiwa na serikali kufuta Mitahani ya Kidato cha pili ilhali hawa waliomaliza wakiwa kidato cha pili  (Form two) ili kutoyaibua hayamapema ile na serikali kuoekana kushindwa kusudio lake hivyo kuamua kuwapitisha kiholela ili yanapokuja tokea yaliyotokea wao watakuwa madarakani tena na kwa hilo wamefanikiwa. Ila hofu yangu kubwa ni kwamba tuliwapitisha kiholela na kidogo wamejua "How are you," Je? s\Si hawa ndio wataongoza mapinduzi ya kisiasa miaka ijayo ama ndo kama CULTURE ya Mtanzania kusahau? Sitaki waza kwa niaba ya wengine kuhusu hili ila tu  nilikua nataka toa angalizo kuwa "MPANGO WA SASA NI KUJENGA ZAHANATI ZA KATA, JE? NA ZENYEWE SI ZITAUA KAMA SHULE ZA KATA ZILIVYOFELISHA?

TUONANE MUNGU AKIPENDA.

Sunday 9 January 2011

HAPPY BIRTHDATE DADA AJUNA.



Malkia wa familia from Left Dada Ajuna, Mama na Dada Ninsiima.

God gave a gift to the world when you were born—
a person who loves, who cares,
who sees a person’s need and fills it,
who encourages and lifts people up,
who spends energy on others
rather than herself,
someone who touches each life she enters,
and makes a difference in the world,
because ripples of kindness flow outward
as each person you have touched, touches others.
Your birthday deserves to be a national holiday,
because you are a special treasure
for all that you’ve done.
May the love you have shown to others
return to you, multiplied.
I wish you the happiest of birthdays,
and many, many more,
so that others have time to appreciate you
as much as I do.


Instead of counting candles,
Or tallying the years,
Contemplate your blessings now,
As your birthday nears.


Consider special people
Who love you, and who care,
And others who’ve enriched your life
Just by being there.


Think about the memories
Passing years can never mar,
Experiences great and small
That have made you who you are.


Another year is a happy gift,
So cut your cake, and say,
"Instead of counting birthdays,
I count blessings every day!"

Happy Birthdate Dada Ajuna
WE LOVE TOU OUR DEAR SISTER.

Wednesday 5 January 2011

HAPPY BIRTHDATE SWEET DADY.




Kwanza namshukuru Maanani kwa kuweza kutuvusha mwaka uliopita na kutufikisha mwaka huu wa 2011. Ni mengi sana tumepitia ambayo si kwa uweza wetu bali ni kwa nguvu zake tumewaza uona mwaka huu.

Pia nipende kumshukuru Mungu kwa kunipa wazazi hawa na hapa nianDikapo napenda  kukupongeza sana Baba kwa kukumbuka siku yako ya kuzaliwa.

Sisi kama wanao twajivunia sana kuwa nawe na Mama, umetufunza mengi ambayo sasa twaonekana kuwa kioo katika jamii na hata yanayotufanya kuishi vizuri na wenzetu ilhali tukiendeleza ule "UPENDOmlioturithisha. Twajivunia kuwa na Wazazi kama nyinyi na twawaombea Baraka zaidi na maisha marefu ili muwezeona nini matunda ya malezi meme kwa wanenu katika yale mliowafundisha. WE WILL ALWAYS BE PROUD OF YOU  na kwa pamoja twakutakia heri na fanaka katika kuikumbuka siku yako hii ya kuzaliwa.


“It is a wise father who knows his own child.” 
                      William Shakespeare.

SWEET DADY.

HAPPY BIRTHDATE BABA.