Thursday 13 October 2011

HAPPY BIRTHDAY SUPER PAULINA.


The Little Angle (Napenda sana kumuita MAMA)
Ni jambo la pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukulinda hadi leo hii uadhimishapo miaka miwili tangu kuzaliwa kwako. Hakika ni safari ndefu ila twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake na hata kuweza fikia hapa.

Pia nitumie fursa hii kipekee kuwakaribisha sana Nyumbani Bukoba Tanzania Wewe (PAU) na Mama Pia.
Mama na Mwana. Karibuni Sana Bukoba wapendwa.
Twafurahi sana kujumuika nanyi katika sherehe hii na kuwa nanyi katika kipindi chote tutachobahatika kuwa nanyi.
 Hakika ni furaha sana kwetu sisi kama Familia na hata kwa kila mmoja wetu kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda safarini mpaka kuwafikisha salama na pia kuwashukuru ninyi kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali hadi kufikia Azma yenu ya kufika huku. Ujio wenu ni ishara tosha ya upendo wenu kwetu na si twaahidi kushirikiana nanyi katika kipindi chote tutachokuwa nanyi.
The Super Parents with their Angel P.A.B
Hivyo basi twawapenda na kuwaombea muwe na Afya tele na amani kwa kipindi chote tutakachokuwa nanyi huku tukimwombea pia kaka yetu Mubelwa (Baba Pau) azidishiwe afya njema na Baraka kwa kipindi choote tutakachokuwa nanyi na hata baada ya Hapo.

KARIBUNI SANA TANZANIA,

KARIBUNI SANA BUKOBA  MAMA PAULINA  NA PAULINA. 

Na mwisho niseme
HAPPY BIRTHDAY Pauliana Arianna Bandio. 

BARAKA KWENU NYOOTE.

1 comment:

  1. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU PAU...NATUMAINI URAFIKI WETU HAUJAISHA AU RAFIKI... HAYA HUKO BUKOBA KLA SANA NDIZI NA KULA KWA NIABA YANGU PIA.MPIA HONGERA SANA WAZAZI/WALEZI.

    ReplyDelete